SIMBA, AZAM ZAMGOMBEA LAMECK LAWI WA COASTAL UNION
Taarifa nilizozipata kutokea Mkoani Tanga ni kwamba mlinzi kitasa wa Coastal Union, Lameck Lawi ana mkataba wa miaka miwili na mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Kwa maana hiyo Azam FC na Simba SC zimeonyesha nia ya kumhitaji nyota huyo watalazimika kuvunja mkataba wa nyota huyo jambo ambalo Coastal Union wanajiandaa kuvuta mkwanja mrefu kwelikweli kama ilivyokuwa Kwa Bakari Nondo na Abdul Sopu.