RASMI PACOME KUWAVAA TABORA UNITED KESHO
Baada ya Kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha ni rasmi Kiungo Pacome Zouzoua amefanya mazoezi jana pamoja na wachezaji wenzake kujiandaa na mchezo dhidi ya Tabora United siku ya Jumatano.
Pacome aliumia katika mchezo was Ligi Kuu bara dhidi ya Azam FC ambapo Yanga ililala kwa mabao 2-1 na tangu alipoumia hajaonekana tena huku kukiwa na kila aina ya fununu zinazovuma juu yake