BARBARA HATIHATI KURUDI SIMBA
Klabu ya Simba SC imeanza mchakato wa kumtafuta CEO mpya baada ya Iman Kajula kujiuzulu siku chache zilizopita.
Barbara Gonzalez amekataa kurudi ndani ya klabu ya Simba baada ya Mangungu kukataa kujiuzulu. Mangungu amesema hawezi kujiuzulu sababu yeye amechaguliwa na wanachama na amesema wasubirie mpaka mkutano mkuu wa Wanachama
Simba imepanga kutangaza mabadiliko ya safu ya uongozi baada ya msimu huu kumalizika.
Viongozi wa Klabu ya Simba bado wanaimani na kocha wao Benchikha na wamemuahidi kumpa ushirikiano kwa mechi zilizobaki na kuanzia msimu ujao