MGUNDA KUMRITHI BENCHIKHA
Kocha wa timu ya wanawake ya Simba Queens Juma Mgunda anatajwa kuchukua mikoba ya kocha wa timu ya wanaume ya Simba SC Abdelhak Benchikha raia wa Algeria.
Mapema leo kocha Benchikha amedaiwa kuachana na Simba na ametangaza kurejea kwao Algeria.
Kocha huyo hana furaha akiwa na kikosi hicho hivyo anataka kuachana na timu hiyo, Mgunda anatajwa kuchukua nafasi kwani kuna ukweli kwamba Benchikha amevunja mkataba.
Mgunda sasa atasaidiwa na Seleman Matola na tayari viongozi wa klabu hiyo wameshafanya mazungumzo na Mgunda