SIMBA MABINGWA WA MUUNGANO

Hatimaye Simba SC imefanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe la Muungano baada ya usiku huu kuifunga Azam FC bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa New Amaan mjini Zanzibar.

Hilo litakuwa taji la pili kwa Simba msimu huu baada ya kutwaa Ngao ya Jamii lakini ni taji la kwanza kwa kocha Abdelhak Benchikha.

Bao pekee la Wekundu hao wa Msimbazi limefungwa dakika ya 78 na kiungo mkabaji Babacar Sall, Simba iliutawala mchezo huo na kama si bahati mbaya ingeweza kupata ushindi mkubwa tangu mapema.

Kitendo cha Azam kumkosa mshambuliaji wake hatari Mzimbabwe Prince Dube kuliifanya timu hiyo kuwa dhaifu na kuwafanya Simba kutokuwa kwenye hatari kubwa


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA