SIMBA YAAMKIA MUUNGANO
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC usiku huu wametakata baada ya kuifunga KVZ mabao 2-0 katika michuano ya Ligi ya Muungano kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mabao ya Simba yamefungwa na Freddy Michael dakika ya 25 na Israel Mwenda dakika ya 90 aliyefunga kwa mkwaju wa penalti.
Kwa maana hiyo Simba imeingia fainali na emdapo itafanikiwa kushinda ubingwa itakuwa rasmi bingwa mpya wa muungano na kuambulia shilingi milioni 50