MAPYA: KOCHA WA KMC KUINOA SIMBA MSIMU UJAO
Licha ya kudaiwa Juma Mgunda anaweza kumrithi kocha Benchikha aliyevunja mkataba.
Simba SC inaangalia uwezekano wa kumpata Kocha Mkuu wa KMC, Abdi Himid Moalin kwenda kocha wa Mkuu wa timu hiyo mpaka mwisho wa msimu huu.
Na uongozi tayari upo kwenye mazungumzo ya kumshawishi msomali huyo kuchukua mikoba ya Abdelhak Benchikha ambae anajiandaa kuachana na timu hiyo muda wowote kuanzia sasa.
Inaelezwa kuwa Abdelhak Benchikha hatokuwa sehemu ya timu itakayosafiri kuelekea Ruangwa kwenye mchezo wao dhidi ya Namungo FC.