MDAKA MISHALE WA ZESCO KUTUA AZAM FC
Inaelezwa kuwa Azam FC inamfuatilia Kwa karibu kipa wa Zesco United ya Zambia Ian Otieno raia wa Kenya mwenye umri wa miaka 30.
Mlinda mlango huyo ndiye atakaenda kuchukua ya mlinda mlango wa sasa wa Azam FC, Mohamed Mustafa.
Mostafa Mohamed anadaiwa kurejea kwenye klabu yake ya El Merreikh mwishoni mwa msimu baada ya kumaliza mkataba wake mkopo ndani ya Chamazi.