AZAM YAIFUATA SIMBA FAINALI YA LIGI YA MUUNGANO
Timu ya Azam FC usiku huu imetinga fainali ya michuano ya Ligi ya muungano baada ya kuilaza KMKM mabao 5-2 katika uwanja wa New Amaan Zanzibar.
Kwa ushindi huo sasa Azan itacheza fainali na Simba SC ambao katika mchezo wake jana iliifunga KVZ mabao 2-0, kwa vyovyote mchezo huo wa fainali utakuwa wa aina yake kutokana na timu hizo kukamiana vikali.
Mabao ya Azam yamefungwa na Abdul Sopu (mawili), Nathaniel Chilambo, Iddi Nado na Iddi Kishindo