MGUNDA AKARIBISHWA NA SARE YA 2-2
Timu ya Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi imeilazimisha sare ya mabao 2-2 Wekundu wa Msimbazi, Simba SC mchezo wa Ligi Kuu bara uliofanyika uwanja wa Majaliwa mjini Ruangwa.
Simba walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia Willy Onana dakika ya 33 kabla ya Namungo kisawazisha kupitia Kevin Sabato dakika ya 39, hadi mapumziko timu hizo zilifungana 1-1.
Kipindi cha pili Simba waliandika bao la pili kupitia Edwin Balua dakika ya 70 kabla ya Namungo kisawazisha dakika ya 89 hasa baada ya kipa wa Simba kujifunga.
Kwa matokeo hayo Simba inaendelea kusalia nafasi ya tatu ikiwa na pointi 47 ikicheza mechi 22, matumaini ya kukwea nafasi ya pili ili ipate tiketi ya kushiriki Ligi ya mabingwa Afrika msimu ujao ni ngumu kwani Yanga na Azam zipo juu yake.
Hii ni mechi ya Kwanza kwa kocha Juma Mgunda aliyechukua nafasi ya Abdelhak Benchikha aliyetangaza kuachana na klabu hiyo