GUEDE AISOGEZA YANGA KARIBU NA UBINGWA
Bao pekee lililofungwa kipindi cha pili na mshambuliaji wa kati Joseph Guede raia wa Ivory Coast limeiwezesha klabu ya Yanga kuondoka na pointi zote tatu baada ya kuifunga bao 1-0 Coastal Union ya Tanga mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa Azam Complex jijini Dar ea Salaam.
Kwa ushindi huo Yanga inaendelea kuongoza ligi hiyo ikifikisha pointi 62 na michezo 24 ikizidi kuziacha nyuma wapinzani wake Azam FC na Simba SC ambazo zinakutana kwenye mchezo wa fainali ya kombe la Muungano huko Zanzibar usiku huu.
Hata hivyo Coastal Union imefungwa bao kipindi cha pili tena ni baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu beki wake Lameck Lawi baada ya kumshika Stephanie Aziz Ki