YANGA PRINCESS YAKUBALI TENA KICHAPO KWA SIMBA QUEENS


Simba Queens imeendeleza ubabe wa Ligi Kuu ya wanawake (WPL) mbele ya Yanga Princess kwa kuifunga tena mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Mabao ya Simba Queens yaliwekwa kimiani na Asha Mnunka katika dakika ya 49 na 90 kumfanya afikishe mabao 15 kwenye ligi nyuma ya kinara Stumai Abdallah mwenye mabao 17, huku bao la tatu leo likifungwa na Jentrix Shikangwa katika dakika ya 66 na kumfanya afikishe mabao matano. Bao la kufutia machozi la Yanga limefungwa na Mmarekani Kaeda Wilson. 

Simba imeifunga Yanga mara mbili kwenye ligi msimu huu ikiipiga kwa idadi ya mabao hayo hayo ambayo straika wake Mnunka aliwafunga mabao mawili-mawili katika kila mechi na hivyo kuiwezesha Queens kuifunga Princess jumla ya mabao 6-2.

Timu hizo mbili kwenye dakika 10 za mwanzo kipindi cha kwanza na pili zilionyesha ushindani wa aina yake na kila timu ilifika langoni kwa mwenzie lakini Simba ilikuwa bora zaidi katika dakika 30 za mwisho.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA