LOMALISA AOMBA KUONDOKA YANGA


Beki wa kushoto klabu ya Yanga, Joyce Lomalisa ameupa taarifa Uongozi wa klabu ya Yanga kuwa anahitaji kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu ambapo atakuwa Mchezaji huru ( Free agent ).

Licha ya kupewa ofa na klabu ya Yanga ya mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuwatumikia Wananchi, amesisitiza kuondoka na ana ofa 3 rasmi kubwa zaidi kutokana klabu za Morocco, Libya na Tanzania.

Kutokana na hilo klabu ya Yanga itaingia sokoni hivi karibuni katika dirisha lijalo la uhamisho ili kupata mchezaji ambaye atajiunga na klabu hiyo kuongeza nguvu eneo la pembeni.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA