CHAMA AWATULIZA WANASIMBA
Kiungo Mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama, amewasihi mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuwapa moyo wachezaji licha ya kikosi chao kupitia wakati mgumu.
Simba SC hivi sasa imekuwa ikipitia kipindi kigumu, ambapo imeshatolewa katika michuano miwili mikubwa huku katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa imepitwa Pointi kadhaa na kinara Young Africans.
“Hata sisi tunaumia kutokana na kipindi hiki tunachopitia kwa sasa. Ni kipindi cha mpito kwetu, tutakaa sawa na kuendelea kuwapa furaha (mashabiki), kikubwa ni kuhakikisha mashabiki wanatusapoti vya kutosha tuweze kufanya vizuri,” amesema CHAMA.
Leo Simba itajitupa uwanjani kusaka Kombe la Muungano mbele ya Azam uwanja wa New Amaan Stadium Zanzibar