SIMBA YAANZA NA MOHAMED CAMARA
Taarifa zilizonifikia zinaeleza kuwa tayari Simba SC imefikia makubaliano na Hafia FC ya nchini Guinea juu ya kumsajili kiungo Mohamed Damaro Camara raia wa Guinea.
Nyota huyo atajiunga na Simba SC kwenye dirisha kubwa la usajili na anatajwa kuwa anakuja kutibu tatizo la eneo la kiungo wa chini ndani ya Msimbazi.
Na tayari Hafia wamekamilisha usajili wa kiungo mwengine Ibrahima Sory Camara kwa ajijili ya kuziba pengo la Mohamed Damaro Camara.