BENCHIKHA KUACHIA NGAZI MWISHONI MWA MSIMU HUU
Inaarifiwa kwamba kocha mkuu was Simba SC Muargeria Abdelhak Benchikha yuko mbioni kuachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu ikidaiwa anataka kutunza heshima yake.
Tangu kocha huyo ajiunge na Simba, hadhi yake inazidi kuporomoka na hasa kutokana na matokeo mabaya inayopata klabu hiyo.
Mpaka sasa Simba imeshatolewa katika michuano ya Ligi ya mabingwa, kombe la FA na pia kuondoka kwenye mbio za kuwania ubingwa wa Tanzania bara
Michuano pekee ambayo Simba inaweza kuambulia kombe ni ligi ya Muungano ambayo imetangazwacm kuanza na TFF