TUMEJIPANGA KUSHINDA- MATOLA
Kocha msaidizi wa Simba SC Seleman Matola amejinasibu kushinda kwenye mchezo wa fainali ya kombe la Muungano utakaofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar Jumamosi.
Simba itacheza na Azam ambapo Mstola amedai itakuwa mechi ngumu ambapo lolote linaweza kutokea, lakini Simba itaibuka na ushindi.
"“Itakuwa mechi ngumu, Azam ni timu bora lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.
Hii ni fainali na siku zote haiwezi kuwa nyepesi kwahiyo tumejipanga kuwakabili.”- amesema kocha Msaidizi, Seleman Matola.