KITUNDA AKABIDHIWA STAND UNITED
Na Prince Hoza
Kocha wa zamani wa timu ya Korosho ya Tunduru mkoani Ruvuma, Seleman Kitunda amekabidhiwa kikosi cha Stand United ya Shinyanga na sasa amepewa majukumu ya kuipandisha daraja msimu ujao.
Kocha huyo anasaidiwa na Kitwana Tambwe ambao wote wamepewa majukumu ya kuhakikisha timu hiyo inarejea Ligi Kuu bara msimu ujao.
Kitunda na Tambwe wameanza kazi hivi karibuni lakini wote kwa pamoja wanahakikisha timu hiyo inamaliza Ligi kwenye nafasi nzuri