HANS PLUIJM KUIBUKIA KENGOLD


Kocha wa Zamani wa Yanga na Singida Big stars Hans Van Der Pluijm ameonyesha hamu ya kutaka Kurejea Tanzania na kuhudumu kama mkurugenzi wa Ufundi kwenye klabu ya Ken Gold FC ambayo Imejihakikishia kushiriki ligi kuu ya Tanzania Bara msimu ujao wa 2024/25.

Kupitia chapisho lake kwenye ukurasa wake wa kijamiii wa Facebook Kocha Pluijm aliandika "Nawapa pongezi klabu ya Ken Gold FC , Ndio naweza kufanya kazi lakini kama mkurugenzi wa Ufundi kusaidia walimu"Ameandika Pluijm akijibu moja ya swali alipoulizwa kama anaweza Kurejea Tanzania kufundisha soka.

Pluijm ni Mwalimu wa Soka mwenye Uzoefu mkubwa na Soka la Tanzania Kwa zaidi ya Miaka 5 amehudumu kwenye Vilabu tofauti kuanzia kama kocha mkuuu akiwa Yanga, lakini aliwahi kuhudumu kama Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi akiwa na Singida Big stars.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA