SIMBA QUEENS YASHUSHA VIPIGO LIGI YA WANAWAKE
JKT Queens imekubali kichapo cha kizalendo cha 2-0 kutoka Kwa Simba Queens katika mchezo wa lIgi Kuu ya Wanawake Tanzania bara uliopigwa Leo na kuifanya Simba Queens kufikisha alama 37 na kuwaacha mbali zaidi JKT Queens wenye alama 28.
Hapo awali JKT Queens ilikumbana na adhabu ya kupokwa alama Tano mara baada ya kutopeleka Timu Uwanjani hapo ndipo paliopanzia kuwepo na ugumu Kwa JKT Queens kutetea ubingwa.
Ikiwa ni raundi ya 13 ya Ligi mpaka sasa matumaini ni madogo Kwa JKT Queens kutetea ubingwa wao huku ukilinganisha na kasi ambayo Simba Queens wamekuwa nayo.