GAMONDI ASEMA HAWAENDI UWANJANI KUSHINDA MABAO MATANO
Kocha wa Yanga SC Miguel Angel Gamondi amesema hawajawahi kutoka Avic Town na wakasema wanaenda kushinda mabao matano isipokuwa inategemeana na makosa ya mpinzani wao.
“Hatujawahi kutoka kambini tukasema tunakwenda kuwafunga wapinzani mabao matano, kushinda mabao mengi inategemea na makosa gani mpinzani ameyafanya dhidi yetu, tuna staili ya soka letu namna ya kutafuta ushindi, kitu muhimu kwetu ni kushinda kwa kupata pointi tatu na kucheza soka la kuvutia,”
.
“Angalia mechi ya juzi ingewezekana kushinda mabao mengi, wapinzani wetu walijua wanakuja kukutana na timu gani wakaamua wote kucheza nyuma ya mpira bado haikuwa shida tulitawala mchezo na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga.”