Usilolijua kaka yake Mbwana Samatta kumbe kwipandisha Ligi Kuu Kengold
Kaka wa Mbwana Samatta, Mohamed Samatta amesaidia kuipandisha Daraja la Ligi Kuu Bara msimu ujao timu ya Ken Gold ya Mbeya.
Mohamed Samatta anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji alikuwa na msimu bora na kikosi hicho katika Mashindano ya Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) msimu huu.
Kabla ya kiungo huyo hajajiunga na timu hiyo amewahi kuzitumikia timu za Mbeya City, KMC, Mbagala Market na African Lyon.