Alikiba achekelea Crown Fm kucheza nyimbo za Diamond Platinumz
Mmiliki wa redio ya Crown Fm Alikiba amefurahishwa na kitendo cha redio yake kucheza nyimbo za hasimu wake Diamond Platinumz, Kiba ambaye naye ni msanii wa bongofleva amefurahishwa na maamuzi hayo na kuandika katika kurasa wake.
"Nimefurahishwa sana baada ya kuona radio yangu ikicheza nyimbo za Diamond Platnumz. Ndio maana nilipokuwa nikiifungua media yangu nikasema hii ni ya kila mtu na si ya familia."
"Crown Fm itacheza nyimbo za Diamond na Harmonize bila kubagua. Natamani pia Wasafi Media wafanye hivyo kwa wasanii wengine."
Alikiba akieleza jinsi alivyofurahishwa na kuchezwa kwa nyimbo za Diamond Platnumz na Harmonize kwenye radio yake.