PRINCE DUBE AANDALIWA MKATABA WA MIAKA MITATU YANGA
Taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam zinasema kuwa mshambuliaji anayejiandaa kuachana na klabu yake ya Azam, ameandaliwa mkataba mnono na klabu moja ya kariakoo kwa ajili ya kuitumikia msimu ujao.
Taarifa za uhakika ni kuwa mshambuliaji huyo ataendelea kusalia nchini na ataendelea kuuwasha katika ligi kuu NBC Tanzania akiwa na kigogo mmoja wa kariakoo.
Prince Dube ameandaliwa mkataba wa miaka mitatu na vigogo hao wa kariakoo na muda wowote atalipa faini kwa klabu yake ya Azam ili awe huru kusaini katika klabu anayoipenda.
Vigogo hao ambao wamepania kufanya vizuri zaidi katika michuano ya kimataifa na kuvuka hatua ambayo wamekwama kuvuka ya robo fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika.