BIL 19.7 KUKARABATI UWANJA WA UHURU "SHAMBA LA BIBI"
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia wizara ya utamaduni Sanaa na michezo imesaini mkataba wa ukarabati na kampuni ya CRCEG ya China kwa ajili ya ukarabati wa uwanja wa Uhuru uliopo jijini Dar es salaam.
Katika hafla ya utiaji wa saini za mkataba huo Serikali imeweka wazi gharama itakayotumika kukarabati uwanja huo ni bilioni 19.7 za Kitanzania na ukarabati huo utachukua miezi 12 sawa na mwaka mmoja.
Hongera Serikali kwa hatua hii ambayo inatoa mwanga kuelekea michuano ya Kombe la mataifa Ya Afrika 2027 ambayo Tanzania,Kenya na Uganda ndio watakuwa wenyeji kwa pamoja.