SIMBA YAMWEKEA MKATABA WA MWAKA MMOJA SIMBA
Klabu ya Simba ilimuwekea mkataba wa mwaka mmoja Kiungo wao Mshambuliaji, Clatous Chama kuendelea kuitumikia klabu hiyo hadi June 2025 kwakuwa mkataba wake na Wekundu wa Msimbazi unamalizika mwishoni mwa msimu huu.
Clatous Chama ana ofa rasmi 3 zilizopo kwenye Menejiment yake, ofa zilizopo ni kutoka klabu ya Simba, Yanga na Red Arrows na ofa anayoipa kipaumbele zaidi ni ofa kutoka Yanga kuanzia vipengele vya kimkataba zaidi ya Simba.
Menejiment ya Clatous Chama itakaa mezani na mteja wao ili kuangalia ni ofa ipi anastahili kuipokea na kusaini kandarasi kuelekea msimu ujao, bado Menejiment haifanya maamuzi ya mwisho pia maamuzi ya mwisho yatafanyika hivi karibuni.