JKT TANZANIA NA YANGA HAKUNA MBABE
Timu ya JKT Tanzania jioni ya leo imeibana mbavu Yanga SC baada ya kuilazimisha sare ya bila kufungana 0-0 katika uwanja wake wa nyumbani wa Meja Isamuya nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Bahati haikuwa yao vijana wa JKT Tanzania kwani tangu kipindi cha kwanza waliutawala mchezo lakini washambuliaji wake wakiongozwa na Matheo Antony, Sixtus Sabilo na Shiza Kichuya wakishindwa wenyewe.
Yanga ambayo katika mzunguko wa kwanza waliifunga mabao 5-0, leo imeshindwa kabisa kuonesha kiwango chao kwani haijafanya lolote na zaidi ingepoteza mchezo