EDO KUMWEMBE AWASHANGAA SIMBA KUCHEKELEA KUFUNGWA NA YANGA GOLI CHACHE

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Edo Kumwembe awechana klabu ya Simba akisema ni aibu kubwa kufurahia kufungwa bao chache na watani zao Yanga Sc.

Edo amesema hayo baada ya Simba kukubali kichapo cha bao 2-1 huku hofu yao ilikuwa ni kufungwa bao nyingi kama ilivyokuwa duru ya kwanza kutokana na ubovu qa kikosi chao.

“Sasa msimu umemalizika dhahiri kwa Simba. Sioni namna gani Simba wakichukua ubingwa kwa pengo la pointi lililopo. Baada ya Azam kucheza dakika 90 na za nyongeza dhidi ya Mashujaa bila ya kufunga bao lolote Ijumaa usiku sioni namna gani Yanga wanaweza kuzuiwa wasitwae ubingwa.

“Swali ni namna gani Simba watarudi msimu ujao. Wamejifunza kitu au wataendelea kumdharau Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said? Watafumua kikosi chao cha utawala wa timu? Watarekebisha mipango yao ya usajili wa timu na kuleta wachezaji wenye hadhi ya Simba katika kikosi? Ni suala la kusubiri kwa sasa..

“Tupo Aprili. Mvua zinanyesha. Tusubiri Aprili ya mwakani kuona Simba itakuwa wapi. Kuona itakuwa imejirekebisha wapi.

Leo ni aibu kuona baadhi ya mashabiki wa Simba wakiwa wanapumua baada ya kufungwa na Yanga. Kisa? Eti wamefungwa mabao machache kuliko walivyotazamia. Aibu,” amesema Edo Kumwembe


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA