Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2018

Ronaldo naye afungashwa virago na Ureno yake

Picha
Hatimaye sasa wachezaji nyota duniani Lionel Messi wa Argentina na Cristiano Ronaldo wa Ureno hatutawaona tena katika fainali za kombe la dunia baada ya timu zao kutolewa. Argentina ilipokea kichapo cha mabao 4-3 na Ufaransa na baadaye Ureno ikaondoshwa na Uruguay kwa mabao 2-1, mchezo huo wa Ureno na Uruguay ulipigwa uwanja wa Olimpiki Fisht mjini Sochi huko Urusi ulishuhudia Uruguay ikitangulia kupata bao kupitia kwa Edinson Cavani dakika ya 7. Goli hilo lilidumu hadi kipindi cha pili pale Pepe alipoisawazishia Ureno kwa kichwa dakika ya 55 kabla ya Cavani tena kuweka mpira kambani dakika ya 62 na kumfanya Ronaldo ashindwe kutimiza ndoto zake za kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo mwaka huu na asubiri labda Qatar mwaka 2022

UFARANSA YAITUPA NJE ARGENTINA NA MESSI WAO HADI HURUMA

Picha
Mabingwa wa dunia wa mwaka 1998 Ufaransa jioni ya leo imefanikiwa kuingia robo fainali ya kombe la dunia baada ya kuilaza Argentina kwa mabao 4-3 mbele ya staa na nahodha wao Lionel Messi. Mchezo ulikuwa mkali na wa kusisimua na iliwachukua dakika 13 Ufaransa kuandika bao la kuongoza lililofungwa na Antoine Griezman kwa mkwaju wa penalti kufuatia Kyilian Mbappe kuangushwa eneo la hatari. Goli hilo halikudumu kwani Argentina walisawazisha kupitia Di Maria dakika ya 43 timu hizo hadi zinaenda mapumziko zikiwa sare, kipindi cha pili Argentina waliandika bao la pili kupitia kwa Gabriel Mercardo dakika ya 48 goli ambalo nalo halikudumu kwani Ufaransa walikomboa kupitia kwa Benjamin Pavard. Kyilian Mbappe ambaye leo alikuwa katika kiwango bora aliweza kufunga mabao ya ushindi moja dakika ya 64 na lingine dakika 68 kabla ya Sergio Aguero hajafunga la tatu kwa upande wa Argentina dakika ya 90, mechi nyingine itapigwa saa 3 usiku kati ya Ureno na Uruguay

Salamba afungua akaunti ya mabao, Simba ikiifumua Dakadaha 4-0

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Mabingwa wa Tanzania bara Simba Sc mchana wa leo imeanza vema michuano ya kombe la Kagame baada ya kuilaza Dakadaha ya Somalia mabao 4-0 mchezo wa kundi C uwanja wa Uhuru Dar es Salaam na kukamata usukani wa kundi hilo. Ikichezesha karibu wachezaji wake wapya iliowasajili hivi karibuni kama Paschal Wawa, Adam Salamba na wengineo ilianza kuandika bao la kwanza kupitia kwa Marcel Kaheza aliyesajiliwa kutoka Majimaji ya Songea dakika ya 14 kabla ya Adam Salamba kufunga la pili dakika ya 23. Dakadaha hawakuonyesha ushindani wowote wakajikuta wanapigwa la tatu dakika ya 45 likifungwa na Rashid Juma, Simba iliandika bao la nne lililofungwa tena naSalamba dakika ya 76 na kufanya iibuke na ushindi huo mnono

16 BORA KOMBE LA DUNIA PANACHIMBIKA LEO, UFARANSA NA ARGENTINA, UINGEREZA NA URENO NA HISPANIA

Picha
Dunia itasimama kwa muda leo pale hatua ya 16 bora ya kombe la dunia itakapoanza kutimua vumbi nchini Urusi kuelekea robo fainali, mabingwa wa dunia mwaka 1998 Ufaransa wanashuka dimbani kuumana na wana fainali wa mwaka 2014 Argentina yenye staa mwenye jina duniani Lionel Messi. Ugumu wa mchezo huo unatokana na Argentina kuingia katika hatua hiyo kibahatibahati kwani ilishindwa kutamba, lakini pia taifa lenye maneno mengi kuhusu mechi nyingine Hispania  itaumana na Ureno ambao hivi karibuni walishangaza kwa kuilaza Senegar na kuitupa nje katika mashindano hayo. Michuano hiyo itaendelea tena kesho Jumapili kwa mechi mbili pia wenyeji Urusi wakiumana na Hispania lakini Ureno yenye staa mwenye jina kubwa duniani Cristiano Ronaldo itakwaruzana na Uruguay ambao wako vizuri sana

SIMBA KUUMANA NA DAKADAHA LEO MCHANA KWEUPE

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Mabingwa wa soka Tanzania bara Simba Sc saa nane mchana inatelemka uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuumana na Dakadaha ya Somalia katika mchezo wa kundi C kombe la Kagame. Simba huenda ikawatumia wachezaji wake wapya iliowasajili hivi karibuni, wachezaji ambao huenda wakatumika leo ni pamoja na mlinda mlango mzoefu Deogratus Munishi "Dida" aliyekuwa Pretolia ya Afrika Kusini, Meddie Kagere wa Gor Mahia ya Kenya na Paschal Wawa aliyekuwa El Marreikh ya Sudan. Wengine ambao pia wamesajili na wanaweza kucheza leo ni Adam Salamba, Marcel Kaheza na Mohamed Rashid, timu ya Singida United ndio vinara wa kundi C baada ya jana usiku kuilaza APR ya Rwanda mabao 2-1, mechi nyingine leo ni kundi B Ports ya Djibout itaumana na Lydia Ludik ya Burundi uwanja wa Azam Complex saa 10 jioni, michuano hiyo ilianza rasmi jana kwa timu za JKU ya Zanzibar na Viper ya Uganda kuumana

TIMU ZA TANZANIA ZAANZA KWA KISHINDO KAGAME CUP

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Wawakilishi wa Tanzania Bara katika michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati maarufu kombe la Kagame zimeanza vema baada ya leo Azam Fc na Singida United kila moja kutoka na ushindi. Mechi ya kwanza ilianza kwa wawakilishi wa Zanzibar, timu ya JKU ikianza kwa sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa kundi A uliopigwa uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam, mchezo huo ulipigwa saa nane mchana. Baadaye saa 10 jioni mabingwa watetezi Azam Fc ilianza vema kampeni yake baada ya kuilaza Kator ya Sudan mabao 2-1, magoli yote ya Azam yamefungwa na Shaaban Iddi Chilunda. Usiku huu Singida United imeanza vema michuano hiyo baada ya kuilaza APR ya Rwanda mabao 2-1, magoli ya Singida United yamefungwa na Habibu Kyombo dakika ya 7 na Tibar John dakika ya 82 wakati lile la APR limefungwa na Akizimana Muhadji. Singida United sasa inaongoza kundi C lenye timu za Simba na Dakadaha ya Somalia ambazo kesho zinaumana saa 8:00 mchana katika uwanj...

YANGA NAO WAJIPANGA KUILIZA SIMBA WIKIENDI HII

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Baada ya Simba kufanikiwa kuwapoka wachezaji watano ambao Yanga ilikuwa ikitaka kuwasajili kwa ajili ya msimu ujao, hatimaye kamati ya usajili ya klabu hiyo iliyo chini ya mwenyekiti wake Abbas Tarimba imejipanga kujibu mapigo. Licha kwamba Simba jana kuweka wazi kuwa itaachana na beki wake Mganda, Juuko Murushid lakini wamempeleka nchini Afrika Kusini kujiunga na Supersport, taarifa za ndani kabisa  zinasema beki huyo alienda Afrika Kusini kufanya majaribio tu na anarejea kimya kimya nchini kutazama michuano ya Kagame lakini ameshafanya mazungumzo na viongozi wa Yanga. Murushid anadaiwa atasaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na mabingwa hao wa zamani na huenda akawa miongoni mwa wachezaji wataoshiriki katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo Yanga itaumana na Gor Mahia, nafasi ya Murushid kucheza Yanga ni kubwa kwani tayari Simba wameshamsaini Paschal Wawa raia wa Ivory Coast ambaye anakuwa mrithi wa Murushid katika kikosi c...

SINGIDA UNITED KUONYESHANA UMWAMBA NA APR

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati maarufu kombe la Kagame inatarajia kuanza leo kwa michezo mitatu, lakini mechi ya kwanza inaendelea kuchezwa muda huu katika uwanja wa Azam Complex Chamazi kundi A JKU ya Zanzibar na Viper ya Uganda. Kipute kingine kitakuwa jioni saa 10:00 kati ya Azam Fc ambao ni mabingwa watetezi wataumana na Kator  ya Sudan katika uwanja huo huo wa Azam. Usiku ndio itapigwa mechi kali kati ya APR ya Rwanda na Singida United uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo ambao unaanza saa 1: usiku, Singida United imeingia katika mashindamo hayo ikichukua nafasi ya Yanga iliyojitoa na APR nayo imeingia ikichukua nafasi ya Saint George ya Ehiopia iliyojitoa

TUNISIA YAONDOA AIBU, UINGEREZA YALALA

Picha
Wawakilishi wa bara la Afrika, Tunisia wameonja ushindi kombe la dunia baada ya ushindi wake wa mabao 2-1 dhidi ya Panama mchezo wa kundi G. Mabao ya ushindi yamefungwa na Fakhreddine Ben Youssef dakika ya 51 na Wahbi Khazri dakika ya 66 wakati lile la Panama ambao walikuwa wa kwanza kufunga liliwekwa kimiani na Rodriguez dakika ya 33, licha ya ushindi huo Tunisia imeaga sambamba na Panama nakuziachia Uingreza na Ubelgiji kusonga. Ubelgiji nao wameifunga Uingereza bao 1-0 lililofungwa na AdnanJanuzaj dakika ya 51 na kuwafanya wamalize kundi G wakiwa kileleni kwa kufikisha pointi tisa, hatua ya 16 bora inaanza Jumamosi

AFRIKA FUNGU LA KUKOSA KOMBE LA DUNIA, SENEGAR YAAGA KWA KICHAPO

Picha
Bara la Afrika limeshindwa kuingiza hata timu moja katika hatua ya 16 bora ya kombe la dunia nchini Urusi baada ya wawakilishi wake watano wote kuaga katika hatua ya makundi. Senegar ambao pekee ndio waliokuwa wakipewa nafasi ya kufuzu hatua ya mtoano imechapwa bao 1-0 uwanja wa Samara Arena Urusi mchezo wa kundi H. Bao ambalo limeitupa nje Senegar limefungwa na beki Yerry Mina dakika ya 74, Senegar sasa inaungana na Poland kuyaaga mashindano hayo licha kwamba nayo imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Japan, mataifa ya Afrika ambayo nayo yametolewa ni Misri, Morocco, Nigeria na Tunisia

Dinno Manyuti aachia "Sina bahati"

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayekuja juu kwa sasa Dinno Manyuti ametambulisha wimbo wake mwingine mpya uitwao "Sina bahati" na umepokelewa vizuri katika vituo mbalimbali vya redio hapa jijini Dar es Salaam. Huu ni wimbo wake wa pili mfululizo baada ya kutambulisha wimbo wake mwingine uliobamba sana "Bado upo" ambao pia aliufanyia video iliyotikisa mitandaoni, Manyuti amedhamiria kufikia mafanikio ya wasanii wa levo za juu hapa nchini akimtaja Diamond Platinumz. Msanii huyo aliibukia katika studio za Burn Record akiwa chini ya prodyuza Shedy Clever miaka ya 2014 lakini hakupata mafanikio kabla ya kuamua kuachana na prodyuza huyo na kutoka kivyake ambapo sasa ameanza kukubalika na watu mbalimbali

Senegar kuibeba Afrika leo? Uingereza na Ubelgiji ni kusuka au kunyoa

Picha
Timu ya taifa ya Senegar leo itabeba mioyo ya mashabiki wa soka barani Afrika katika shindano la kombe la dunia huko nchini Urusi pale itakaposhuka uwanjani kuumana na Colombia mchezo wa kundi H uwanja wa Samara Arena, Urusi. Senegar ndio wawakilishi pekee wa Afrika waliosalia katika michuano hiyo wakiongoza katika kundi hilo, lakini bado nafasi ya kutinga 16 bora kwao inaweza kuwa ngumu iwapo itapoteza mchezo huo na Japan itaishinda Poland katika uwanja wa Volgograd Stadium. Mechi nyingine za kundi G leo ni kati ya Uingereza na Ubelgiji wakati Panama itaumana na Tunisia ambazo zote zimeshatolewa

Brazil hawataki mchezo mchezo wawabutua Serbia 2-0, Uswisi na Costa Rica sare

Picha
Magoli yaliyofungwa na Paulinho na Thiago Silva yametosha kabisa kuwapa ushindi wa mabao 2-0 timu ya taifa ya Brazil katika mchezo wa kundi E kombe la dunia. Ushindi huo unaivusha Brazil kutinga hatua ya mtoano ya 16 bora na sasa itaumana na Mexico katika hatua hiyo, Pia timu ya taifa ya Uswisi nayo imeungana na Brazil baada ya kutoka sare Costa Rica 2-2 na sasa itaumana na Sweden katika hatua ya mtoano. Michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi nne kama kawaida, kundi H Japan itaumana na Poland wakati Senegar na Colombia nalo kundi G Uingereza itaumana na Ubelgiji na Tunisia itajiuliza kwa Panama

Simba yaendelea kuiliza Yanga, yamsajili Dida miaka miwili

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Hii sasa sifa kwa mabingwa wa soka nchini Simba Sc leo kufanikiwa kumsajili aliyekuwa kipa wa Yanga Deogratus Munishi "Dida" kwa mkataba wa miaka miwili na sasa atasimama langoni katika michuano ya Kagame Cup inayoanza Ijumaa. Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Simba Sc, Haji Sunday Manara amesema Simba imemsajili kipa huyo aliyekuwa anacheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini katika klabu inayomilikiwa na chuo kikuu ya daraja la pili. Dida alitua nchini kwa ajili ya mapumziko lakini alikuwa akitakiwa na Yanga ambao walikuwa wakifanya naye mazungumzo, lakini Simba imeweza kumalizana naye na leo kuingia naye mkataba, usajili huo wa Dida ni baada ya ule wa jana kumsainisha straika wa Gor  Mahia ya Kenya, Meddie Kagere. Dida ni kama amerejea nyumbani kwani kabla ya kujiunga na Mtibwa Sugar, Azam Fc na Yanga Sc, Dida alikuwa anaichezea Simba Sc iliyomsajili akitokea Ashanti ya Ilala

Akina Honda waivua ubingwa Ujerumani

Picha
Ujerumani imevuliwa ubingwa wa kombe la dunia leo baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Korea Kusini katika mchezo wa kundi F uwanja wa Kazan Arena, Urusi. Mabao ya Korea Kusini yamefungwa na Kim Young Gwon dakika ya 90 za kawaida lingine Son Heung Min dakika sita za nyongeza na kusababisha Ujerumani kuvuliwa taji lake ililolitwaa mwaka 2014 nchini Brazil baada ya kuilaza Argentina 1-0 katika fainali. Pia Ujwrumani inakuwa imetolewa kwa mara ya kwanza kuanzia hatua ya makundi baada ya miaka 80, Ujerumani na Korea Kusini zote zimeaga mashindano hayo na kuzipisha Sweden na Mexico kutinga hatua ya 16 bora. Sweden nayo imeichapa Mexico mabao 3-0 yaliyofungwa na LudwigAugustinsson dakika ya 50, Andreas Grangvist kwa penalti dakika ya 52 na Edson Alvarez aliyejifunga mwenyewe dakika ya 74, usiku huu Brazil inaumana na Serbia wakati Colombia inaumana na Costa Rica

Brazil na Serbia ni roho mkononi, Ujerumani na Korea Kusini kazi ipo

Picha
Huenda historia ikajirudia kwa miamba Brazil kukutana tena na Ujerumani kwenye hatua ya mtoano ya 16 bora iwapo leo hii miamba hiyo itakapofanikiwa kutinga hatua hiyo. Katika kundi E Brazil inaumana na Serbia uwanja wa Spartak mjini Moscow na Uswisi itaumana na Costa Rica uwanja wa Nizhni Novgorod Arena. Nafasi bado ngumu kwa Brazil kwani Serbia na Uswisi nao wana nafasi ya kutinga 16 bora. Vita nyingine ipo kundi F wakati mabingwa watetezi Ujerumani wakiumana na Korea Kusini uwanja wa Kazan Stadium hiyo itakuwa saa 3 usiku na pia Mexico itaumana na Sweden, pia nafasi ni ngumu kwa Ujerumani kufuzu hatua ya 16 bora kwani hata Sweden ina nafasi, tayari Mexico imeshafuzu 16 bora

Argentina yajipigia Nigeria, Croatia yawa mbabe kundi D

Picha
Magoli mawili yaliyofungwa na Lionel Messi dakika ya 14 na Marcos Rojo dakika ya 86 yametosha kabisa kuipa ushindi Argentina na kutinga hatua ya 16 bora kombe la dunia kundi D uwanja aa Saint Petersburg mjini Moscow baada ya kuifunga Nigeria mabao 2-1. Bao la Nigeria la kufuta machozi lilifungwa na Victor Moses kwa mkwaju wa penalti dakika ya 51, Nigeria imetupwa nje ya mashindano hayo. Croatia nayo imeibuka mbabe kundi D baada ya kuilaza Iceland mabao 2-1 uwanja wa Roston On Don Arena, mabao ya Croatia yamefungwa na Milan Badelj dakika ya 53 na Ivan Perisic dakika ya 90 na lile la Iceland lilifungwa na Gylfi Sigurdsson dakika ya 76 kwa mkwaju wa penalti Croatia wanamaliza mechi zote tatu wakiibuka wababe baada ya pia kuzishinda Nigeria na Argentina na kufikisha alama 9

FUNDI WA MPIRA SHAABAN KIPRESHA, AJIKITA KWENYE UKOCHA MDAULA

Picha
Na Ayubu Mhina. Pwani Kwa wakazi wa Mdaula kata ya Bwilingu, Chalinze wilayani Bagamoyo wanamfahamu vema kwa jina la Shaaban Hussein Kipresha akiwa kama mkufunzi wa Mdaula United. Kipresha amewahi kulisakata kabumbu la ushindani jijini Dar es Salaam, mwenyewe anasimulia kuwa amewahi kukipiga Jah People ya Magomeni Mikumi mtaa wa Ifunda, Baghdad pia ya Makuti mtaa wa Shoka sambamba na Big Bonn ya mtaa huo huo, anadai akiwa Big Bonn amecheza na wakali kama Habib Mahadhi, Khalid Ngome, Gidion Kaburi, Dyson Abiola na wengineo lakini alipokuwa Baghdad alicheza na Godfrey Kalumbeta, Hamza Mtaalamu na Jah People amecheza na George Kavila. Kipresha alikuwa akicheza namba nane yaani kiungo, anawakumbuka sana akina Athuman Machupa, Jabir Aziz "Stima", Shekhan Rashid na wengineo ambao anakiri aliwafunika vilivyo lakini bahati haikuwa yake na akajikuta anaangukia mtaani na sasa ni kocha wa Mdaula United ya Mdaula inayoshiriki Ligi Daraja la tatu Pwani. Kipresha tayari amehitimu kozi ...

PERU YAONJA USHINDI KOMBE LA DUNIA, UFARANSA IKIBANWA NA DENMARK LAKINI ZASONGA 16 BORA

Picha
Timu ya taifa ya Peru leo jioni imeonja ushindi wake wa kwanza katika michuano ya kombe la dunia nchini Urusi kundi C baada ya kuifunga Australia mabao 3-0 na kuambulia pointi tatu licha kwamba imetupwa nje. Ushindi huo unadaiwa ni historia kwao kwani wana miaka 40 hawakuwahi kupata ushindi kwenye fainali kama hizo, mabao ambayo yamewapa ushindi yamefungwa na Andre Carrillo dakika  ya 18 na nahodha mpambanaji Paolo Guerrero dakika ya 50. Ufaransa nayo imeshindwa kufurukuta mbele ya Denmark baada ya kutoka suluhu 0-0 mchezo wa kundi C uwanja wa Luzhiniki mjini Moscow, usiku huu zinapigwa mechi nyingine mbili Argentina ikichuana na Nigeria uwanja wa Saint Petersburg na Croatia na Iceland uwanja wa Rostov On Don Arena

HATIMAYE KAGERE ASAINI SIMBA MIAKA MIWILI

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda mwenye adili ya Uganda leo amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam akitokea Gor Mahia ya Kenya. Kagere amesaini mbele ya Rais wa Simba Salim Abdallah "Try Again" na moja kwa moja ataungana na wachezaji wenzake kambini kujiandaa na michuano ya kombe la Kagame inayotarajia kuanza Alhamisi ijayo. Kagere pia alikuwa akiwaniwa na Yanga Sc, mshambuliaji huyo aliibuka mfungaji bora katika mashindano ya Sportpesa Super Cup iliyofanyika nchini Kenya na timu yake ya Gor Mahia ilibeba kombe kwa kuilaza Simba mabao 2-0 katika mchezo wa fainali magoli yakifungwa na Kagere na Jacques Tuyisenge

KAGERE ATUA KUMALIZANA NA SIMBA

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Mabingwa wa Tanzania Bara, Simba Sc hawatanii kwenye masuala ya usajili baada ya kufanikiwa kumshusha mazoezini Muivory Coast, Paschal Wawa Serge ambaye pia alikuwa akitakiwa na mahasimu wao Yanga, Simba wamemleta straika wa Gor Mahia ya Kenya, Mnyarwanda Meddie Kagere. Kahere alitua nchini jana tayari kabisa kwa ajili ya mazungumzo na Simba na mambo yakienda vizuri anamwaga wino kuitumikia klabu hiyo katika michuano mbalimbali msimu ujao. Kagere ameambatana na wakala wake na mipango ikienda sawia basi atavaa jezi za rangi nyekundu na nyeupe zinazovaliwa na klabu hiyo, Kagere alikuwa akitajwa pia kujiunga na Yanga, lakini Yanga wameshindwa kutoa milioni 180 alizokuwa akihitaji nyota huyo, Mohamed "Mo" Dewji ameamua kumleta ili kumsainisha, pia Simba inaweza kumalizana na straika Victor Patrick kutoka Nigeria

SARE SARE MAUA ZATAWALA KUNDI C KOMBE LA DUNIA, SASA NI VITA 16 BORA

Picha
Raundi ya tatu imemalizika leo usiku kwa kundi C kombe la dunia ambapo sare zimetawala katika mechi zote mbili na hatimaye kuzipeleka timu za Hispania na Ureno katika hatua ya 16 bora ambayo ni ya mtoano. Hispania ilienda sare ya kufungana mabao 2-2 na Morocco wakati Ureno nayo ikienda sare ya 1-1 na Iran ambapo mshambuliaji Cristiano Ronaldo akikosa penalti. Sasa ratiba ya hatua ya mtoano tayari imejulikana ambapo Ureno itachuana na Uruguay wakati Hispania itacheza na mwenyeji Urusi

URUGUAY YAIKUNG' UTA URUSI 3-0, SAUDI ARABIA YAIUMBUA MISRI NA SALAH WAO HADI HURUMA

Picha
Mabao matatu yaliyofungwa na Luis Suarez dakika ya 10, Denis Sheryshev dakika ya 23 na Edison Cavani dakika ya 90 yametosha kuipa ushindi wa mabao 3-0 Uruguay dhidi ya wenyeji Urusi na kuwafanya waibuke vinara kundi A. Matokeo hayo yamewafanya kufikisha pointi 9 ikishika nafasi ya kwanza, mchezo mwingine Saudi Arabia i imeizamisha Misri mabao 2-1 na kuwafanya wafikishe pointi tatu huku Misri ikiwa timu iliyotia aibu kwenye kundi A ikifungwa mechi zote tatu na kurudi bila hata pointi moja, mabao ya Saudi Arabia yamefungwa na Salman Al Faraj dakika ya 45 na Salem dakika ya 90 wakati lile la Misri lilifungwa na Mohamed Salah dakika ya 22. Usiku huu kutapigwa mechi nyingine mbili Ureno na Iran wakati Hispania na Morocco

SIMBA YAMSHUSHA WAWA MAZOEZINI, KUCHEZA KAGAME

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Simba Sc wameifanyia unyamamkubwa Yanga Sc ambap ni mahasimu wao wa jadi baada ya kuwazunguka kwa nyuma na kumnasa beki kisiki wa El Merreikh ya Sudan ambaye aliwahi kucheza katika klabu ya Azam Fc, Paschal Wawa Serge raia wa Ivory Coast. Beki huyo amewasili nchini na leo amehudhuria mazoezi ya klabu hiyo Boko Veterani, Wawa ameungana nawacjezaji wenzake na taarifa zinasema kuwa atatumika katika michuano ya Klabu bingwa Afrika mashariki na kati maarufu Kagame Cup na akiwini atapewa mkataba. Beki huyo ilikuwa asajiliwe na Yanga lakini wameshindwa kunleta nchini na wenzao wamefanikiwa kumleta na inasemekana atasaini mkataba wa miaka miwili, nafasi ya Wawa ni ya Laudit Mavugo ambaye anajiunga na KMC au Mbao Fc

Kispoti

Picha
Musonye na CECAFA yenu mnaishi dunia gani? Na Prince Hoza MICHUANO ya Klabu bingwa Afrika mashariki na kati maarufu kombe la Kagame inatarajia kuanza mwishoni mwa mwezi huu hapa nchini na jumla ya timu 12 zimepangwa katika makundi matatu ambapo timu nane zitavuka hadi robo fainali, michuano hiyo itapigwa katika viwanja viwili tofauti, Uwanja wa Taifa na Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam. Katibu mkuu wa kudumu wa Baraza la vyama vya soka Afrika mashariki Nicholaus Musonye amesema michuano ya Klabu bingwa Afrika mashariki na kati maarufu kombe la Kagame itafanyika Tanzania Bara na viwanja viwili vitatumika, Musonye alianza kutambulisha mchezo kati ya Simba Sc na Yanga Sc ambao ni mahasimu wa soka la Tanzania kwamba zitaumana Julai 5. Musonye alisema Simba na Yanga zimepangwa kundi C, aidha Musonye aliweka wazi makundi yote matatu ambapo kila kundi lilikuwa na timu nne, Tanzania Bara inawakilishwa na timu tatu ambazo ni Yanga Sc, Simba Sc na Azam Fc, Musonye amedai Yanga imein...

Ni vita ya Cristiano Ronaldo leo, Waarabu kuonyeshana umwamba nao

Picha
Leo kutakuwa na mechi nne za mwisho kumaliza mzunguko wa tatu wa fainali za kombe la dunia kabla hatua ya mtoano haijaanza. Hispania na Morocco zenyewe zitaumana usiku wa saa 3 sambamba ma Iran na Ureno mechi ambayo itakuwa ikimuhusu Cristiano Ronaldo ambaye anakitaka kiatu cha dhahabu kwa udi na uvumba ili avunje rekodi ya ufungaji,hadi sasa Ronaldo ana mabao manne akizidiwa moja na Harry Kane wa Uingereza ambaye ana mabao matano. Mechi nyingine leo ni Saudia Arabia na Misri ambao watachuana saa 11 jioni sawa na Urusi na Uruguay zote zikipigwa muda huo huo ili kuhofia kupanga matokeo, jana usiku timu ya Colombia iliifunga Poland mabao 3-0

Honda atibua ushindi wa Senegar dhidi ya Japan, Uingereza yaua Panama

Picha
Goli la kusawazisha lililofungwa kunako dakika ya 78 na mchezaji aliyeingia kipindi cha pili Honda limetibuasherehe za ushindi kwa Senegar baada ya kutoka sare na Japan mabao 2-2 usiku huu kombe la dunia Urusi. Senegar ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na Sadio Mane dakika ya 11 kabla ya Inui hajaisawazishia Japan, Senegar walipata bao la pili kupitia kwa Wague dakika ya 70 lakini Honda akachomoa na kuwa 2-2 timu zote sasa zinakbana koo kileleni zote zikiwa na pointi 4. Jioni ya leo Uingereza imsichapa Panama mabao 6-1 uwanja wa Stadion Nizhny Novgorrod,mabao matatu pekee yamefungwa na Harry Kane dakika za 22, 45 na 62 yote kwa penalti, mengine John Stones dakika ya 8 na 40 na lingine limefungwa na Jesse Lingard dakika ya 36 na lile la Panama limefungwa na Felipe Baloy  dakika ya 78, usiku wa saa 3 Poland itaumana na Colombia

Bocco awa mchezaji bora wa mwaka VPL

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Nahodha na mshambuliaji wa Simba Sc John Raphael Bocco amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana usiku katika hafla maalum iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Bocco aliwabwaga Emmanuel Okei na Erasto Nyoni wote wa Simba SC na kutunukiwa shilingi Milioni 12, tuzo ya mchezaji wa heshima ilienda kwa Edward Akwitende aliyewahi kuichezea Taifa Stars mwaka 1952 hadi 1954, bao bora limeenda kwa Shaaban Iddi Chilunda wa Azam Fc. Kikosi bora ni Aisha Mamula, Hassan Kessy,Shafiq Batambuze, Erasto Nyoni, Kelvin Nyoni, Papy Tshishimbi, Shiza Kichuya, Tafadzwa Kutinyu, Bocco, Emmanuel Okwi na Marcel Kaheza. Mwamuzi bora Heri Sasii, mwamuzi bora msaidizi Hellan Mduma, kocha bora Mohamed Abdallah wa Prisons, timu yenye nidhamu Mtibwa Sugar,mchezaji bora chipukizi wa Ligi Kuu Bara, Habibu Kiyombo wa Mbao Fc, mchezaji anayechipukia Ismail Khalfan Award ni Abuu Juma wa Mtibwa Sugar, kipa bora Aishi ...

Ujerumani yaibanjua Sweden 2-1 na kufufua matumaini

Picha
Mabingwa watetezi wa kombe la dunia timu ya taifa ya Ujerumani imefufua matumaini ya kutetea taji lake baada ya kuizamisha Swedsm mabao 2-1 uwanja wa Sochi Arena. Sweden walikuwa wa kwanza kulata bao la kuongoza lililofungwa dakika ya 32 na Ola Toivonen kabla ya Marco Reus kuisawazishia Ujwrumani na Toni Kroos kufunga la ushindi dakika ya 90. Kwa ushindi huo Ujerumani imefufua matumaini ya kutetea taji ikifikisha pointi tatu sawa na Sweden nayo yenye pointi kama hizp, mechi zao za mwisho zitaamua nani aingie hatua ya 16 bora

Kaseja adaiwa kujiunga na KMC

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Mlinda mlango wa Kagwra Sugar Juma Kaseja anadaiwa amemalizana na uongozi wa timu iliyopanda Ligi Kuu Bara KMC yenye maskani yake Kinondoni jijini Dar es Salaam. Taarifa za Kaseja kutua KMC zinasema kuwa kipa huyo amesaini mkataba wa miaka miwili na ataitumikia timu hiyo msimu ujao, Kaseja ni mali ya KMC kwani hakuwa na mkataba wa Kagwra Sugar alikuwa anacheza tu kilisema chanzo chetu cha habari. Kaseja ni kipa mkongwe hapa nchini aliyepata kuzichezea Simba na Yanga pamoja na Mbeya City pia aliwahi kuichezea Moro United na timu ya taifa,Taifa Stars kwa nyakati tofauti

Mexico yaikung' uta Korea Kusini 2-1, Ubelgiji yaipondaponda Tunisia 5-2

Picha
Timu ya taifa yaMexico jioni ya leo imejiweka pazuri baada ya kuichapa Korea Kusini mabao 2-1 mchezo wa kundi F. Mabao ya Mexico ambayo sasa imefikisha pointi sita na kukata tiketi ya kuingia hatua ya mtoano yamefungwa na Carlos Vela kwa mkwaju wa penalti dakika ya 26 na lingine likifungwa na Xaviel Hernandez dakika ya 66 wakati lile la Korea Kusini limefungwa na Song Heung dakika ya 90. Katika mchezo ulioanza saa 9 alasiri, Ubelgiji yenyewe imeipondaponda Tunisia kwa mabao 5-2 na kuitupa nje mashindanoni, mabao ya Ubelgiji yamefungwa na Romelu Lukaku aliyefunga mawili, Eden Hazard pia mawili na Michy Batshuayi moja, na yale ya Tunisia yamefungwa na Dylan Bronn na Khazil, mechi nyingine inapigwa usiku huu kati ya Ujerumani na Sweden

Tunisia kuibeba Afrika leo? Ujerumani kusuka au kunyoa

Picha
Fainali za kombe la dunia zinazidi kupamba moto ambapo leo zinapigwa mechi tatu katika viwanja tofauti, wawakilishi wa bara la Afrika, Tunisia wanakipiga na Ubelgiji uwanja wa Spartak mchezo ukipigwa saa 9;00 alasiri. Tunisia inahitaji ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri, saa 12 00 jioni Korea Kusini wataumana na Mexico uwanja wa Roston On Don Arena kukamilisha raundi ya pili kundi E. Lakini kundi G itapigwa mechi saa 3:00 usiku ambapo mabingwa watetezi Ujerumani itaumana na Sweden uwanja wa Sochi Stadium, Ujerumani inahitaji kushinda ili iweze kufufua matumaini ya kutetea taji lake kwani katika mchezo wake wa kwanza ilifungwa 1-0 na Mexico

USWISI YACHOMOA BAO NA KUPIGA LA PILI IKIILAZA SERBIA

Picha
Timu ya taifa ya Uswisi ama watunza fedha za ulimwengu usiku wa leo wamefanya maajabu ya aina yake baada ya kusawazisha bao na kuongeza la pili na la ushindi ambalo ssas limewafanya kuwa sawa na Brazil zote zikiwa na pointi nne. Uswisi wameweza kuishinda Serbia mabao 2-1 mchezo wa kundi E ukipigwa uwanja wa Kaliningrad Arena nchini Urusi. Walikuwa Serbia kuanza kupata bao kubako dakika ya 5 kupitiakwa Mitrovic kabla ya Granit Xhaka kuisawazishia Uswisi dakika ya 52 kisha Xherdan Shaqiri kuongeza la pili dakika ya 90

MTIBWA SUGAR YAIBOMOA KAGERA SUGAR

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro imeibomoa Kagera Sugar baada ya kumnasa kiungo mshambuliaji Jaffar Kibay kwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili. Usajili huo ni sehemu ya kukiimarisha kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao pia ni matayarisho yake kwa ajili ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani. Akizungumzia usajili huo Afisa habari wa Mtibwa Sugar, Tobias Kifaru amesema ujio wa Kibaya ndani ya kikosi hicho ni kama amerejea tena nyumbani kwani aliwahi kuichezea Mtibwa kabla hajajiunga na Kagera Sugar

NIGERIA YAFUFUA MATUMAINI YA WAAFRIKA, BRAZIL YAANZA NA MOTO

Picha
Timu ya taifa ya Nigeria imefufua matumaini ya kutinga hatua ya mtoano baada ya kuichapa Iceland mabao 2-0 na kuifanya ifikishe pointi tatu ikihitaji sare katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Argentina. Mabao yote ya Nigeria yamewekwa kimiani na mshambuliaji wake Ahmed Musa kunako dakika ya 49 na 75. Nayo Brazil ilifufua kasi yake baada ya kuichapa Costa Rica mabao 2-0 mchezo ukipigwa uwanja wa Saint Petersburg. Alianza Philipe Coutinho kuifungia Brazil bao la kuongoza dakika ya 90 kabla ya Neymar Dos Santos kufunga la pili katika dakika saba za nyongeza, kwa matokeo hayo Brazil inafikisha pointi nne, mchezp mwingine leo unatarajia kuanza saa tatu kati ya Uswisi na Serbia

Kimenuka, Leonarda na Sony Lava wamwagana

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba video vixen Leonarda Wolper na mwimbaji na mtunzi wa mashairi Sebastian "Sony Lava" ambao walikuwa wakiishi pamoja kama mke na mume hatimaye wamwagana. Leonarda Wolper amesema jana kwamba ameamua kuachana na Sony Lava ambaye hivi karibuni alitambulisha video yake ya "Na wewe"  aliyomshirikisha Leonarda katika video kwa madai amekuwa akimtangaza vibaya kwa watu. Leonarda amesema kwamba Sony Lava amekuwa akijisifu kwa marafiki zake kuwa yeye ni mke wake kitu ambacho si kweli, "Mimi na Sony Lava ni marafiki tu na wala siyo wapenzi kama anavyojitamba, siwezi kutoka naye hata mara moja namchukulia kama kaka yangu". alisema Leonarda. Alipoulizwa Sony Lava kuhusu kuachana na Leonarda akakiri ni kweli wameachana lakini alidai alikuwa mkewe na si rafiki kama anavyosema, "Leonarda ni kama mke wangu tumeishi wote zaidi ya mwaka sasa lakini ushamba ndio uliomfanya tuachane, ana mambo ...

BRAZIL NA COSTA RICA NI VITA YA WENYEWE KWA WENYEWE, NIGERIA KUSAKA HESHIMA KWA ICELAND

Picha
Fainali za kombe la dunia za mwaka huu zinazofanyika nchini Urusi zimeanza kuingia kwenye ushindani wa aina yake ambapo tena leo zinapigwa mechi tatu zote zikiwa muhimu. Wawakilishi wa bara la Afrika,Nigeria wanashuka dimbani kwenye uwanja wa Volgograd Arena kuumana na Iceland mchezo wa kundi D ambapo kama itashinda basi inaweza kufufua matumaini ya Waafrika kufuzu hatua ya mtoano. Lakini kundi E litawaka moto mabingwa wa kihistoria Brazil wataumana na ndugu zao Costa Rica uwanja wa Sankt Petersburg,Brazil ilianza kwa sare na Uswisi hivyo inataka ushindi wakati Costa Rica walilala kwa Serbia kwa maana hiyo mechi itakuwa kali. Pambano lingine ni kati ya Serbia na watunza fedha za dunia Uswisi mechi ambayo itapigwa uwanja wa Kaliningrad Arena Kwa habari kamili gonga www.mambouwanjani.blogspot.com

UFARANSA YATANGULIA 16 BORA IKIIBANJUA PERU 1-0, DENMARK IKISHIKWA SHATI NA AUSTRALIA, MESSI ASUBIRIWA NA CROATIA

Picha
Mabingwa wa dunia wa mwaka 1998 Ufaransa wametangulia hatua ya 16 bora ya kombe la dunia kundi C baada ya jioni ya leo kuilaza Peru bao 1-0 katika uwanja wa Ekateringburg Arena nchini Urusi. Goli ambalo limeibeba Ufaransa lilifungwa na kinda Kylian Mbappe dakika ya 34, hata hivyo Mbappe ameingia kwenye rekodi ya kufunga goli katika fainali hizo akiwa na umri mdogo, Mbappe ana miaka 19. Katika mchezo mwingine ulioanza saa tisa alasiri, Denmark imebanwa mbavu na Australia baada kutoka sare ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Samara, goli la Denmark lilifungwa na Christian Eriksen dakika ya 7 na la kusawazisha la Peru lilifungwa kwa mkwaju wa penalti na Mile Jedinak hasa baada ya mchezaji mwenye asili ya Tanzania Yusuf Poulsen kuushika mpira, goli hilo kilifungwa dakika ya 38. Hata hivyo Mtanzania huyo alipewa kadi nyekundu,mchezo mwingine wa kundi D unataraji kupigwa katika uwanja wa Nizhni Novgorod kati ya Argentina na Croatia mechi ambayo itakuwa ni ya maonyesho kwa Lionel Messi

BIASHARA MARA YANASA MAPROO WANNE, SIMBA NA YANGA KAZI MNAYO MSIMU UJAO

Picha
Na Paskal Beatus. Mwanza Timu ya Biashara Mara imeanza kujiimarisha kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kukamilisha usajili wa wachezaji wanne wa kimataifa ambao watawatumia msimu ujao. Meneja wa timu hiyo iliyopanda Ligi Kuu msimu huu Amani Josiah amesema wameamua kusajili wachezaji hao wa kimataifa ni kwa ajili ya msimu ujao na wamepania kufanya vizuri. Josiah amesema kikosi chake mbali na kusajili nyota hao a kigeni pia wamewapandisha wachezaji wa kikosi B pamoja na wale walioipandisha timu kutoka Ligi daraja la kwanza, wachezaji ambao wamesajiliwa ni kipa Balora Nouridine kutoka Burkina Faso, Alex Olumide ambaye ni kiungo kutoka Nigeria. Wengine ni kiungo Wilfred Kouroume kutoka Guinea na mshambuliaji Astin Amos kutoka Ivory Coast, Biashara Mara imepanda Ligi Kuu Bara sambamba na timu za Alliance School ya Mwanza, Coastal Union ya Tanga, African Lyon, JKT Tanzania  na  KMC za Dar es Salaam

UFARANSA NA PERU ITAKUWA SHUGHURI PEVU

Picha
Michuano ya kombe la dunia leo inaendelea tena kwa mechi tatu kupigwa katika viwanja tofauti nchini Urusi,  Ufaransa leo inaumana na Peru katika mchezo wa kundi C uwanja wa Ekaterinburg Arena. Ufaransa inahitaji ushindi wa aina yoyote ili kutinga hatua ya 16 bora ya mtoano, Ufaransa iliishinda Australia mabao 2- 1 wakati Peru ilipoteza dhidi ya Denmark kwa bao 1-0. Mchezo mwingine kundi C ni kati ya Denmark  na Australia ambao unatarajia kuanza kabla ya mechi ya Ufaransa, mchezo wa mwisho utakaopigwa saa 3 usiku ni kati ya Argentina na Croatia utakaopigwa uwanja wa Nizhni Arena utakuwa ni wa kundi D

DIEGO COSTA AIPA USHINDI WA KWANZA HISPANIA DHIDI YA IRAN

Picha
Goli pekee laushindi lililofungwa dakika ya 54 na mshambuliaji Diego Costa leo usiku limetoshakuwapa ushindi wa kwanza kundi B timu ya taifa ya Hidpania wa bao 1-0 dhidi ya Iran mchezo wa kombe la dunia uliopigwa uwanja wa Kazan Arena. Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa hazijafungana hata bao, vijana wa Iran walionekana kuwamudu vema Hispania wenye nyota mbalimbali wanaocheza vilabu vikubwa barani Ulaya. Na kama si mwamuzi wa mchezo huo kulikataa goli la Iran huenda mchezo huo ungemalizika kwa sare na kuiweka Hispania taabani, sasa vita ya kuwania kuingia hatua ya 16 bora ni kati ya Ureno, Hispania na Iran ambapo mechi zao za mwisho zitaamua

SUAREZ, RONALDO WAZIFUNGASHA VIRAGO MISRI NA MOROCCO KOMBE LA DUNIA

Picha
Goli lililofungwa kunako dakika ya 4 kipindi cha kwanza lilitosha kabisa kuipa ushindi wa bao 1-0 timu ya taifa ya Ureno dhidi ya wawakilishi wa Afrika, Morocco na kuifungasha virago katika michuano hiyo mikubwa kabisa duniani. Bao hilo limefungwa na staa Cristiano Ronaldo ambalo limemfanya aendelee kuongoza kwa upachikaji magoli, lakini katika mchezo mwingine uliomalizika hivi punde timu ya taifa ya Uruguay imeungana na Urusi kutinga hatua ya 16 bora baada ya kuilaza Saudi Arabia bao 1-0 goli ambalo lilifungwa dakika ya 23 na mshambuliaji Luiz Suarez na kumfanya atimize bao lake la 100, kwa maana hiyo Misri inakuwa imetolewa rasmi kwakuwa hata kama itashinda mchezo wake wa mwisho haitaweza kusalia Urusi Mchezo mwingine wa mwisho kwa leo unaendelea muda huu kati ya Hispania na Iran mchezo ambao utatoa mwangaza kwenye kundi hilo linaloonekana kuwa gumu hasa kutokana na timu zilizomo kwenye kundi hilo

SERIKALI YAUFUNGIA WIMBO MPYA WA SUGU

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia wimbo mpya wa mwanamuziki na mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Mr Two Sugu unaofahamika kwa jina la Mfungwa au 219 usipigwe wala kuonekana katika chombo chochote cha habari na kwenye kumbi za burudani kwa madai haufai. Mtendaji wa BASATA Geofrey Mngereza amesema baraza lake limeufungia wimbo huo kwakuwa umekosa maadili na unaweza  kuigawa jamii na kusababisha kutoweka kwa amani ya nchi. Sugu aliamua kutunga mashairi ya wimbo huo baada ya kuachiwa kutoka gerezani kwa msamaha wa Rais, lakini wimbo wake huo unadaiwa kuwa na maneno makali yenye kuleta uvunjifu wa amani hapa nchini,  Mngereza amesema Basata imekuwa ikizifungia nyimbo zinazokosa maadili aidha kwa mavazi ama lugha chafu na uchochezi kama ilivyo kwa wimbo huo mpya wa msanii huyo ambaye pia ni mbunge, Sugu ameua kuuita wimbo huo 219 ikiwa ni namba yake alipokuwa mfungwa

Ronaldo kuendeleza moto kwa Morocco leo, Hispania na Iran ngoma inogile

Picha
Raundi ya pili ya kombe la dunia inaendelea leo baada ya jana Misri na wenyeji Urusikucheza mechi zao za pili, mitanange leo itakuwa mitatu ambapp Uruguay iraanza kwa kuumana na Saudi Arabia katika mchezo wa kundi A uwanja wa Rostov Arena. Lakini baadaye Ureno yenye staa wake mahiri duniani Cristiano Rondo yenyewe itashuka dimbani kuwavaa wawakilishi wengine wa Afrika,Morocco katika uwanja wa Luzhniki Arena jijini Noscow, Ronaldo anaongoza kwa magoli akifunga matatu na leo anataka kuendeleza tena rekodi yake ya kutupia. Hispania nayo inaumana na watengeneza nyuklia wa Iran mechi ambayo itakuwa kali na ya kusisimua kutokana na historia ya mataifa hayo wawili kuhusiana kindugu tokea karne zilizopita

Urusi yawa ya kwanza kutinga 18 bora, ikiilowesha Misri 3-1

Picha
Wenyeji Urusi leo usiku wamekuwa wa kwanza kutinga 18 baada ya kuichapa Misri mabao 3-1 mchezo wa kundi A kombe la dunia uwanja wa San Petersburg Arena. Misri wamejiweka pabaya baada ya matokeo hayo kwani tayari wamepoteza mechi mbili na wamesaliwa na mchezo mmoja, Ahmed Fakhy wa Misri alijifunga dakika ya 47 kabla ya Denis Cheeyshev kufunga bao la pili. Smolov Dyzuba akafunga la tatu dakika ya 62 wakati Mohamed Salah akaifungia Misri goli la kufutia machozi kwa mkwaju wa penalti dakika ya 73, Urusi sasa imefikisha pointi 6 na inaongoza katika kundi lake ikifuatiwa na Uruguay yenye pointi tatu wakati Saudi Arabia inamakata mkia ikiwa haina pointi wala bao

Singida United yachukua nafasi ya Yanga kombe la Kagame

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Timu ya Singida United ya mkoani Singida imepewa nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati maarufu kombe la Kagame baada ya Yanga Sc kujitoa katika kinyang' anyiro hicho. Katibu mkuu wa CECAFA Nicholaus Musonye amesema Singida United itashiriki michuano hiyo na imepangwa kundi C walilokuwa Yanga Sc ambao wamejiondoa, Yanga wamejitoa kwa sababu wana mchezo wao wa kombe la Shirikisho barani Afrika na mabingwa wa Kenya, Gor Mahia hivyo wameshindwa kushirikimichuao hiyo. Singida United itaanza kwa kucheza na APR katika uwanja wa Azam Complex Chamazi na kundi lao linahusisha timu nne ambazo ni Simba Sc,  Dakadaha ya Somalia na APR ya Uganda

Senegar yaibeba Afrika kwa kuilaza Poland, Japan nayo hakuna kulala

Picha
Wawakilishi wa bara la Afrika katika michuano ya kombe la dunia nchini Urusi, Senegar imeanza vema baada ya kuichapa Poland  mabao 2-1 katika mchezo wa kundi H uwanja wa Spartak jijini Moscow. Poland walijikuta wanafungwa bao dakika ya 37 na Thiago Cionek kabla ya Niang kufunga la pili dakika ya 60 na dakika ya 86 Grzegorz Krychowiak akaifungia bao la kufutia machozi timu yake ya Poland, hayo ni matokeo mazuri kwa Senegar kwanj imekuwa timu ya kwanza kwa Afrika kushinda. Mchana timu ya taifa ya Japan imeilaza Colombia mabao 2-1 yaliyofungwa na Shinji Kagawa dakika ya 6 na Yuya Osako dakika ya 73 kabla ya Juan Fernando Quintero kufunga la kufutia machozi kwa upande wa Colombia kunako dakika ya 39, mchezo ulifanyika katika uwanja wa Saransk,  usiku huu wenyeji Urusi wanaumana na Misri

Uingereza yaiua Tunisia kwa bao la usiku

Picha
Almanusura Tunisia leo usiku iweke rekodi ya kuwa timu ya kwanza kwa bara la Afrika kupata pointi baada ya kwenda sare na Uingereza hadi dakika ya 90 za mchezo lakini ikalala katika muda wa nyongeza na kufanya matokeo kuwa 2-1 Tunisia ikilala. Uingereza ilitangulia kupata bao la uongozi lililowekwa kimiani na Harry Kane dakika ya 11 kipindi cha kwanza goli ambalo lilidumu hadi dakika ya 35 pale Ferjan Sassi kuisawazishia Tunisia, hadi mapumziko timu hizo zilikuwa nguvu sawa. Kipindi cha pili kilikuwa kigumu kwa kila timu kwani zote zilishambuliana kwa zamu, baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika na mwamuzi kuongeza nne, ndipo Harry Kane alipogeuka shujaa wa Waingereza pale alipofunga bao la pili na la ushindi, leo michuano hiyo inaendelea tena Senegar inaumana na Poland Spartak Moscow Arena, Colombia na Japan Saransk na Urusi inaumana na Misri