Kaseja adaiwa kujiunga na KMC
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Mlinda mlango wa Kagwra Sugar Juma Kaseja anadaiwa amemalizana na uongozi wa timu iliyopanda Ligi Kuu Bara KMC yenye maskani yake Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Taarifa za Kaseja kutua KMC zinasema kuwa kipa huyo amesaini mkataba wa miaka miwili na ataitumikia timu hiyo msimu ujao, Kaseja ni mali ya KMC kwani hakuwa na mkataba wa Kagwra Sugar alikuwa anacheza tu kilisema chanzo chetu cha habari.
Kaseja ni kipa mkongwe hapa nchini aliyepata kuzichezea Simba na Yanga pamoja na Mbeya City pia aliwahi kuichezea Moro United na timu ya taifa,Taifa Stars kwa nyakati tofauti