Ni vita ya Cristiano Ronaldo leo, Waarabu kuonyeshana umwamba nao

Leo kutakuwa na mechi nne za mwisho kumaliza mzunguko wa tatu wa fainali za kombe la dunia kabla hatua ya mtoano haijaanza.

Hispania na Morocco zenyewe zitaumana usiku wa saa 3 sambamba ma Iran na Ureno mechi ambayo itakuwa ikimuhusu Cristiano Ronaldo ambaye anakitaka kiatu cha dhahabu kwa udi na uvumba ili avunje rekodi ya ufungaji,hadi sasa Ronaldo ana mabao manne akizidiwa moja na Harry Kane wa Uingereza ambaye ana mabao matano.

Mechi nyingine leo ni Saudia Arabia na Misri ambao watachuana saa 11 jioni sawa na Urusi na Uruguay zote zikipigwa muda huo huo ili kuhofia kupanga matokeo, jana usiku timu ya Colombia iliifunga Poland mabao 3-0

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA