Tunisia kuibeba Afrika leo? Ujerumani kusuka au kunyoa
Fainali za kombe la dunia zinazidi kupamba moto ambapo leo zinapigwa mechi tatu katika viwanja tofauti, wawakilishi wa bara la Afrika, Tunisia wanakipiga na Ubelgiji uwanja wa Spartak mchezo ukipigwa saa 9;00 alasiri.
Tunisia inahitaji ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri, saa 12 00 jioni Korea Kusini wataumana na Mexico uwanja wa Roston On Don Arena kukamilisha raundi ya pili kundi E.
Lakini kundi G itapigwa mechi saa 3:00 usiku ambapo mabingwa watetezi Ujerumani itaumana na Sweden uwanja wa Sochi Stadium, Ujerumani inahitaji kushinda ili iweze kufufua matumaini ya kutetea taji lake kwani katika mchezo wake wa kwanza ilifungwa 1-0 na Mexico