Dinno Manyuti aachia "Sina bahati"
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayekuja juu kwa sasa Dinno Manyuti ametambulisha wimbo wake mwingine mpya uitwao "Sina bahati" na umepokelewa vizuri katika vituo mbalimbali vya redio hapa jijini Dar es Salaam.
Huu ni wimbo wake wa pili mfululizo baada ya kutambulisha wimbo wake mwingine uliobamba sana "Bado upo" ambao pia aliufanyia video iliyotikisa mitandaoni, Manyuti amedhamiria kufikia mafanikio ya wasanii wa levo za juu hapa nchini akimtaja Diamond Platinumz.
Msanii huyo aliibukia katika studio za Burn Record akiwa chini ya prodyuza Shedy Clever miaka ya 2014 lakini hakupata mafanikio kabla ya kuamua kuachana na prodyuza huyo na kutoka kivyake ambapo sasa ameanza kukubalika na watu mbalimbali