SARE SARE MAUA ZATAWALA KUNDI C KOMBE LA DUNIA, SASA NI VITA 16 BORA
Raundi ya tatu imemalizika leo usiku kwa kundi C kombe la dunia ambapo sare zimetawala katika mechi zote mbili na hatimaye kuzipeleka timu za Hispania na Ureno katika hatua ya 16 bora ambayo ni ya mtoano.
Hispania ilienda sare ya kufungana mabao 2-2 na Morocco wakati Ureno nayo ikienda sare ya 1-1 na Iran ambapo mshambuliaji Cristiano Ronaldo akikosa penalti.
Sasa ratiba ya hatua ya mtoano tayari imejulikana ambapo Ureno itachuana na Uruguay wakati Hispania itacheza na mwenyeji Urusi