Brazil hawataki mchezo mchezo wawabutua Serbia 2-0, Uswisi na Costa Rica sare
Magoli yaliyofungwa na Paulinho na Thiago Silva yametosha kabisa kuwapa ushindi wa mabao 2-0 timu ya taifa ya Brazil katika mchezo wa kundi E kombe la dunia.
Ushindi huo unaivusha Brazil kutinga hatua ya mtoano ya 16 bora na sasa itaumana na Mexico katika hatua hiyo, Pia timu ya taifa ya Uswisi nayo imeungana na Brazil baada ya kutoka sare Costa Rica 2-2 na sasa itaumana na Sweden katika hatua ya mtoano.
Michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi nne kama kawaida, kundi H Japan itaumana na Poland wakati Senegar na Colombia nalo kundi G Uingereza itaumana na Ubelgiji na Tunisia itajiuliza kwa Panama