SERIKALI YAUFUNGIA WIMBO MPYA WA SUGU
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia wimbo mpya wa mwanamuziki na mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Mr Two Sugu unaofahamika kwa jina la Mfungwa au 219 usipigwe wala kuonekana katika chombo chochote cha habari na kwenye kumbi za burudani kwa madai haufai.
Mtendaji wa BASATA Geofrey Mngereza amesema baraza lake limeufungia wimbo huo kwakuwa umekosa maadili na unaweza kuigawa jamii na kusababisha kutoweka kwa amani ya nchi.
Sugu aliamua kutunga mashairi ya wimbo huo baada ya kuachiwa kutoka gerezani kwa msamaha wa Rais, lakini wimbo wake huo unadaiwa kuwa na maneno makali yenye kuleta uvunjifu wa amani hapa nchini, Mngereza amesema Basata imekuwa ikizifungia nyimbo zinazokosa maadili aidha kwa mavazi ama lugha chafu na uchochezi kama ilivyo kwa wimbo huo mpya wa msanii huyo ambaye pia ni mbunge, Sugu ameua kuuita wimbo huo 219 ikiwa ni namba yake alipokuwa mfungwa