PERU YAONJA USHINDI KOMBE LA DUNIA, UFARANSA IKIBANWA NA DENMARK LAKINI ZASONGA 16 BORA
Timu ya taifa ya Peru leo jioni imeonja ushindi wake wa kwanza katika michuano ya kombe la dunia nchini Urusi kundi C baada ya kuifunga Australia mabao 3-0 na kuambulia pointi tatu licha kwamba imetupwa nje.
Ushindi huo unadaiwa ni historia kwao kwani wana miaka 40 hawakuwahi kupata ushindi kwenye fainali kama hizo, mabao ambayo yamewapa ushindi yamefungwa na Andre Carrillo dakika ya 18 na nahodha mpambanaji Paolo Guerrero dakika ya 50.
Ufaransa nayo imeshindwa kufurukuta mbele ya Denmark baada ya kutoka suluhu 0-0 mchezo wa kundi C uwanja wa Luzhiniki mjini Moscow, usiku huu zinapigwa mechi nyingine mbili Argentina ikichuana na Nigeria uwanja wa Saint Petersburg na Croatia na Iceland uwanja wa Rostov On Don Arena