USWISI YACHOMOA BAO NA KUPIGA LA PILI IKIILAZA SERBIA
Timu ya taifa ya Uswisi ama watunza fedha za ulimwengu usiku wa leo wamefanya maajabu ya aina yake baada ya kusawazisha bao na kuongeza la pili na la ushindi ambalo ssas limewafanya kuwa sawa na Brazil zote zikiwa na pointi nne.
Uswisi wameweza kuishinda Serbia mabao 2-1 mchezo wa kundi E ukipigwa uwanja wa Kaliningrad Arena nchini Urusi.
Walikuwa Serbia kuanza kupata bao kubako dakika ya 5 kupitiakwa Mitrovic kabla ya Granit Xhaka kuisawazishia Uswisi dakika ya 52 kisha Xherdan Shaqiri kuongeza la pili dakika ya 90