Bocco awa mchezaji bora wa mwaka VPL
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Nahodha na mshambuliaji wa Simba Sc John Raphael Bocco amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana usiku katika hafla maalum iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Bocco aliwabwaga Emmanuel Okei na Erasto Nyoni wote wa Simba SC na kutunukiwa shilingi Milioni 12, tuzo ya mchezaji wa heshima ilienda kwa Edward Akwitende aliyewahi kuichezea Taifa Stars mwaka 1952 hadi 1954, bao bora limeenda kwa Shaaban Iddi Chilunda wa Azam Fc.
Kikosi bora ni Aisha Mamula, Hassan Kessy,Shafiq Batambuze, Erasto Nyoni, Kelvin Nyoni, Papy Tshishimbi, Shiza Kichuya, Tafadzwa Kutinyu, Bocco, Emmanuel Okwi na Marcel Kaheza.
Mwamuzi bora Heri Sasii, mwamuzi bora msaidizi Hellan Mduma, kocha bora Mohamed Abdallah wa Prisons, timu yenye nidhamu Mtibwa Sugar,mchezaji bora chipukizi wa Ligi Kuu Bara, Habibu Kiyombo wa Mbao Fc, mchezaji anayechipukia Ismail Khalfan Award ni Abuu Juma wa Mtibwa Sugar, kipa bora Aishi Manula, mabingwa wa ligi Simba Sc wamepewa Milioni 96, washindi wa pili Azam Fc wamepata milioni 45, washindi wa tatu Yanga Sc wamepeta milioni 34 na washindi wa nne Prisons wamepata milioni 27