TUNISIA YAONDOA AIBU, UINGEREZA YALALA
Wawakilishi wa bara la Afrika, Tunisia wameonja ushindi kombe la dunia baada ya ushindi wake wa mabao 2-1 dhidi ya Panama mchezo wa kundi G.
Mabao ya ushindi yamefungwa na Fakhreddine Ben Youssef dakika ya 51 na Wahbi Khazri dakika ya 66 wakati lile la Panama ambao walikuwa wa kwanza kufunga liliwekwa kimiani na Rodriguez dakika ya 33, licha ya ushindi huo Tunisia imeaga sambamba na Panama nakuziachia Uingreza na Ubelgiji kusonga.
Ubelgiji nao wameifunga Uingereza bao 1-0 lililofungwa na AdnanJanuzaj dakika ya 51 na kuwafanya wamalize kundi G wakiwa kileleni kwa kufikisha pointi tisa, hatua ya 16 bora inaanza Jumamosi