Ronaldo naye afungashwa virago na Ureno yake

Hatimaye sasa wachezaji nyota duniani Lionel Messi wa Argentina na Cristiano Ronaldo wa Ureno hatutawaona tena katika fainali za kombe la dunia baada ya timu zao kutolewa.

Argentina ilipokea kichapo cha mabao 4-3 na Ufaransa na baadaye Ureno ikaondoshwa na Uruguay kwa mabao 2-1, mchezo huo wa Ureno na Uruguay ulipigwa uwanja wa Olimpiki Fisht mjini Sochi huko Urusi ulishuhudia Uruguay ikitangulia kupata bao kupitia kwa Edinson Cavani dakika ya 7.

Goli hilo lilidumu hadi kipindi cha pili pale Pepe alipoisawazishia Ureno kwa kichwa dakika ya 55 kabla ya Cavani tena kuweka mpira kambani dakika ya 62 na kumfanya Ronaldo ashindwe kutimiza ndoto zake za kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo mwaka huu na asubiri labda Qatar mwaka 2022

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI