SUAREZ, RONALDO WAZIFUNGASHA VIRAGO MISRI NA MOROCCO KOMBE LA DUNIA

Goli lililofungwa kunako dakika ya 4 kipindi cha kwanza lilitosha kabisa kuipa ushindi wa bao 1-0 timu ya taifa ya Ureno dhidi ya wawakilishi wa Afrika, Morocco na kuifungasha virago katika michuano hiyo mikubwa kabisa duniani.

Bao hilo limefungwa na staa Cristiano Ronaldo ambalo limemfanya aendelee kuongoza kwa upachikaji magoli, lakini katika mchezo mwingine uliomalizika hivi punde timu ya taifa ya Uruguay imeungana na Urusi kutinga hatua ya 16 bora baada ya kuilaza Saudi Arabia bao 1-0 goli ambalo lilifungwa dakika ya 23 na mshambuliaji Luiz Suarez na kumfanya atimize bao lake la 100, kwa maana hiyo Misri inakuwa imetolewa rasmi kwakuwa hata kama itashinda mchezo wake wa mwisho haitaweza kusalia Urusi

Mchezo mwingine wa mwisho kwa leo unaendelea muda huu kati ya Hispania na Iran mchezo ambao utatoa mwangaza kwenye kundi hilo linaloonekana kuwa gumu hasa kutokana na timu zilizomo kwenye kundi hilo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA