Mexico yaikung' uta Korea Kusini 2-1, Ubelgiji yaipondaponda Tunisia 5-2
Timu ya taifa yaMexico jioni ya leo imejiweka pazuri baada ya kuichapa Korea Kusini mabao 2-1 mchezo wa kundi F.
Mabao ya Mexico ambayo sasa imefikisha pointi sita na kukata tiketi ya kuingia hatua ya mtoano yamefungwa na Carlos Vela kwa mkwaju wa penalti dakika ya 26 na lingine likifungwa na Xaviel Hernandez dakika ya 66 wakati lile la Korea Kusini limefungwa na Song Heung dakika ya 90.
Katika mchezo ulioanza saa 9 alasiri, Ubelgiji yenyewe imeipondaponda Tunisia kwa mabao 5-2 na kuitupa nje mashindanoni, mabao ya Ubelgiji yamefungwa na Romelu Lukaku aliyefunga mawili, Eden Hazard pia mawili na Michy Batshuayi moja, na yale ya Tunisia yamefungwa na Dylan Bronn na Khazil, mechi nyingine inapigwa usiku huu kati ya Ujerumani na Sweden