HATIMAYE KAGERE ASAINI SIMBA MIAKA MIWILI
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda mwenye adili ya Uganda leo amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam akitokea Gor Mahia ya Kenya.
Kagere amesaini mbele ya Rais wa Simba Salim Abdallah "Try Again" na moja kwa moja ataungana na wachezaji wenzake kambini kujiandaa na michuano ya kombe la Kagame inayotarajia kuanza Alhamisi ijayo.
Kagere pia alikuwa akiwaniwa na Yanga Sc, mshambuliaji huyo aliibuka mfungaji bora katika mashindano ya Sportpesa Super Cup iliyofanyika nchini Kenya na timu yake ya Gor Mahia ilibeba kombe kwa kuilaza Simba mabao 2-0 katika mchezo wa fainali magoli yakifungwa na Kagere na Jacques Tuyisenge