SIMBA KUUMANA NA DAKADAHA LEO MCHANA KWEUPE
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Mabingwa wa soka Tanzania bara Simba Sc saa nane mchana inatelemka uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuumana na Dakadaha ya Somalia katika mchezo wa kundi C kombe la Kagame.
Simba huenda ikawatumia wachezaji wake wapya iliowasajili hivi karibuni, wachezaji ambao huenda wakatumika leo ni pamoja na mlinda mlango mzoefu Deogratus Munishi "Dida" aliyekuwa Pretolia ya Afrika Kusini, Meddie Kagere wa Gor Mahia ya Kenya na Paschal Wawa aliyekuwa El Marreikh ya Sudan.
Wengine ambao pia wamesajili na wanaweza kucheza leo ni Adam Salamba, Marcel Kaheza na Mohamed Rashid, timu ya Singida United ndio vinara wa kundi C baada ya jana usiku kuilaza APR ya Rwanda mabao 2-1, mechi nyingine leo ni kundi B Ports ya Djibout itaumana na Lydia Ludik ya Burundi uwanja wa Azam Complex saa 10 jioni, michuano hiyo ilianza rasmi jana kwa timu za JKU ya Zanzibar na Viper ya Uganda kuumana