BRAZIL NA COSTA RICA NI VITA YA WENYEWE KWA WENYEWE, NIGERIA KUSAKA HESHIMA KWA ICELAND
Fainali za kombe la dunia za mwaka huu zinazofanyika nchini Urusi zimeanza kuingia kwenye ushindani wa aina yake ambapo tena leo zinapigwa mechi tatu zote zikiwa muhimu.
Wawakilishi wa bara la Afrika,Nigeria wanashuka dimbani kwenye uwanja wa Volgograd Arena kuumana na Iceland mchezo wa kundi D ambapo kama itashinda basi inaweza kufufua matumaini ya Waafrika kufuzu hatua ya mtoano.
Lakini kundi E litawaka moto mabingwa wa kihistoria Brazil wataumana na ndugu zao Costa Rica uwanja wa Sankt Petersburg,Brazil ilianza kwa sare na Uswisi hivyo inataka ushindi wakati Costa Rica walilala kwa Serbia kwa maana hiyo mechi itakuwa kali.
Pambano lingine ni kati ya Serbia na watunza fedha za dunia Uswisi mechi ambayo itapigwa uwanja wa Kaliningrad Arena
Kwa habari kamili gonga www.mambouwanjani.blogspot.com