BIASHARA MARA YANASA MAPROO WANNE, SIMBA NA YANGA KAZI MNAYO MSIMU UJAO
Na Paskal Beatus. Mwanza
Timu ya Biashara Mara imeanza kujiimarisha kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kukamilisha usajili wa wachezaji wanne wa kimataifa ambao watawatumia msimu ujao.
Meneja wa timu hiyo iliyopanda Ligi Kuu msimu huu Amani Josiah amesema wameamua kusajili wachezaji hao wa kimataifa ni kwa ajili ya msimu ujao na wamepania kufanya vizuri.
Josiah amesema kikosi chake mbali na kusajili nyota hao a kigeni pia wamewapandisha wachezaji wa kikosi B pamoja na wale walioipandisha timu kutoka Ligi daraja la kwanza, wachezaji ambao wamesajiliwa ni kipa Balora Nouridine kutoka Burkina Faso, Alex Olumide ambaye ni kiungo kutoka Nigeria.
Wengine ni kiungo Wilfred Kouroume kutoka Guinea na mshambuliaji Astin Amos kutoka Ivory Coast, Biashara Mara imepanda Ligi Kuu Bara sambamba na timu za Alliance School ya Mwanza, Coastal Union ya Tanga, African Lyon, JKT Tanzania na KMC za Dar es Salaam