Uingereza yaiua Tunisia kwa bao la usiku
Almanusura Tunisia leo usiku iweke rekodi ya kuwa timu ya kwanza kwa bara la Afrika kupata pointi baada ya kwenda sare na Uingereza hadi dakika ya 90 za mchezo lakini ikalala katika muda wa nyongeza na kufanya matokeo kuwa 2-1 Tunisia ikilala.
Uingereza ilitangulia kupata bao la uongozi lililowekwa kimiani na Harry Kane dakika ya 11 kipindi cha kwanza goli ambalo lilidumu hadi dakika ya 35 pale Ferjan Sassi kuisawazishia Tunisia, hadi mapumziko timu hizo zilikuwa nguvu sawa.
Kipindi cha pili kilikuwa kigumu kwa kila timu kwani zote zilishambuliana kwa zamu, baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika na mwamuzi kuongeza nne, ndipo Harry Kane alipogeuka shujaa wa Waingereza pale alipofunga bao la pili na la ushindi, leo michuano hiyo inaendelea tena Senegar inaumana na Poland Spartak Moscow Arena, Colombia na Japan Saransk na Urusi inaumana na Misri