Simba yaendelea kuiliza Yanga, yamsajili Dida miaka miwili
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Hii sasa sifa kwa mabingwa wa soka nchini Simba Sc leo kufanikiwa kumsajili aliyekuwa kipa wa Yanga Deogratus Munishi "Dida" kwa mkataba wa miaka miwili na sasa atasimama langoni katika michuano ya Kagame Cup inayoanza Ijumaa.
Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Simba Sc, Haji Sunday Manara amesema Simba imemsajili kipa huyo aliyekuwa anacheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini katika klabu inayomilikiwa na chuo kikuu ya daraja la pili.
Dida alitua nchini kwa ajili ya mapumziko lakini alikuwa akitakiwa na Yanga ambao walikuwa wakifanya naye mazungumzo, lakini Simba imeweza kumalizana naye na leo kuingia naye mkataba, usajili huo wa Dida ni baada ya ule wa jana kumsainisha straika wa Gor Mahia ya Kenya, Meddie Kagere.
Dida ni kama amerejea nyumbani kwani kabla ya kujiunga na Mtibwa Sugar, Azam Fc na Yanga Sc, Dida alikuwa anaichezea Simba Sc iliyomsajili akitokea Ashanti ya Ilala