Ujerumani yaibanjua Sweden 2-1 na kufufua matumaini
Mabingwa watetezi wa kombe la dunia timu ya taifa ya Ujerumani imefufua matumaini ya kutetea taji lake baada ya kuizamisha Swedsm mabao 2-1 uwanja wa Sochi Arena.
Sweden walikuwa wa kwanza kulata bao la kuongoza lililofungwa dakika ya 32 na Ola Toivonen kabla ya Marco Reus kuisawazishia Ujwrumani na Toni Kroos kufunga la ushindi dakika ya 90.
Kwa ushindi huo Ujerumani imefufua matumaini ya kutetea taji ikifikisha pointi tatu sawa na Sweden nayo yenye pointi kama hizp, mechi zao za mwisho zitaamua nani aingie hatua ya 16 bora